30 Novemba 2024 - 15:09
Sambamba na uwepo wa watumishi wa Razawi (Imam Reza a.s) huko Shamu (Syria); Vifurushi 10,000 vya misaada ya kujikimu vilisambazwa miongoni mwa wahamiaji wa Lebanon

Vifurushi 10,000 vya misaada ya kimaisha vimesambazwa miongoni mwa Wahamiaji wa Lebanon sambamba na uwepo wa watumishi wa Haram Tukufu ya Imam Ali bin Musa al-Reza (a.s) huko Syria.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Mkuu wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Haram Tukufu ya Razawi (Imam Reza a.s), kando ya usambazaji wa vifurushi vya kujikimu kimaisha nchini Syria, aliashiria zaidi juu ya undani wa hatua hii na kusema:

Paket hizi zinawasilishwa kwa msaada wa Wahudumu, Watumishi, Wafuasi na Wapenzi wa Hazrat Imam Reza (a.s) ambazo zilitayarishwa chini ya Bendera ya kizingiti kitakatifu cha Haram Tukufu ya Razawi, na kutumwa nchini Syria ili kuwasaidia watu wenye hima na bidii wa Lebanon.